MigogoroUlaya
Ukraine: Urusi imetekeleza wimbi jipya la mashambulizi Kyiv
23 Juni 2025Matangazo
Tymur Tkachenko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kyiv amesema watu kadhaa wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi hayo. Hayo yanajiri baada ya Ukraine kuanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi ikilenga miundombinu ya nishati na kijeshi ya Urusi.
Juhudi za kidiplomasia za kumaliza vita hivyo vilivyodumu kwa miaka mitatu zimekwama, huku mkutano wa mwisho wa moja kwa moja kati ya pande hizo mbili ukiwa ulifanyika karibu wiki tatu zilizopita na hadi sasa kukiwa hakuna mazungumzo mengine yaliyopangwa.