Ukraine na Urusi kuanza mazungumzo mapya Jumatano
22 Julai 2025Matangazo
Mkutano huo uliotangazwa jana Jumatattu na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ni muendelezo wa duru nyingine za awali ambazo zilipiga hatua ndogo ya mafanikio katika kuvifikisha mwisho vita kati ya nchi hizo mbili.
Mazungumzo hayo yatafanyika katika mji wa Istanbul nchini Uturuki, mahali kulikofanyika mazungumzo yaliyokwama mnamo mwezi Mei na Juni.
Zelensky aliongeza kusema kwamba taarifa zaidi kuhusu mkutano huo zitatolewa hivi leo. Urusi haikutoa kauli mara moja kuthibitisha duru mpya ya mazungumzo.