UchumiUkraine
Ukraine na Marekani zasaini"makubaliano ya uwekezaji"
1 Mei 2025Matangazo
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi wa Ukraine Yulia Svyrydenko, aliyetia saini makubaliano hayo mjini Washington, amesema vifungu muhimu vya mkataba huo ni pamoja na kwamba rasilimali zote kwenye eneo la Ukraine na eneo la maji ni mali ya Ukraine.
Marekani chini ya makubaliano hayo, inaweza kuchimba madini ya thamani na adimu nchini Ukraine ili taifa hilo liendelee kupata msaada wa Marekani wakati ikiendelea kukabiliana na uvamizi wa Urusi.
Rais wa Marekani Donald Trump ameshinikiza kupatikana kwa makubaliano kwa miezi kadhaa ambayo anasema yatakuwa ni kama malipo kwa Marekani kufuatia msaada wa kijeshi na kifedha ambayo imeipatia Ukraine.