Ujumbe wa Ukraine, bila Zelensky kufanya mazungumzo na Urusi
15 Mei 2025Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky hatashiriki mazungumzo hayo na amesema atautuma ujumbe utakaoongozwa na Waziri wake wa Ulinzi Rustem Umerov.
Rais wa Urusi aliutuma ujumbe wake wa ngazi ya chini. Zelensky ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Ankara kuwa ujumbe huo wa Urusi haujamjuisha yeyote anayeweza kufanya maamuzi.
Soma pia: Wajumbe wa Urusi na Ukraine wawasili Uturuki kwa mazungumzo ya amani
Akizungumza leo kwenye ndege yake ya Air Force One, akiwa njiani kwenda Umoja wa Falme za Kiarabu akitokea Qatar, Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatarajii hatua mafanikio yoyote kwenye mazungumzo hayo hadi pale atakapokutana mwenye na Putin, ambaye hakusafiri kwenda Uturuki. "Hakuna kitu kitakchofanyika hadi mimi na Putin tukae pamoja, sawa? Na ni wazi kwamba hakutaka kwenda Uturuki, lakini alidhani kuwa nitakwenda. Asingeenda kama nisingekuwepo huko. Siamini chochote kitakatokea, upende usipende, hadi tukae meza moja. ikiwa unapenda au la, mpaka yeye na mimi tupate pamoja. Lakini itabidi tupate suluhisho kwa sababu watu wengi sana wanakufa."
Rais Zelensky amesema ameutuma ujumbe wake ili kumdhihirishia Trump kuwa Ukraine inataka kumaliza vita hivyo vya miaka mitatu.