Israel kushiriki mazungumzo ya usitishaji vita Gaza
10 Machi 2025Matangazo
Awamu ya kwanza ya usitisaji wa vita ilimalizika tangu tarehe mosi ya mwezi huu wa tatu bila makubaliano yoyote juu ya hatua zinazofuata ambazo zinaweza kupata suluhisho la kudumu wa vita, lakini pande zote mbili zimejizuia kuanzisha tena mapigano kamili.
Soma pia:Israel kupeleka ujumbe Qatar kuendelea na mazungumzo ya kusitisha vita Gaza
Hamas mara kwa mara imekuwa ikitoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya haraka kuhusu awamu inayofuata, huku Israel ikisimamia msimamo wake wa kurefushwa kwa awamu ya sasa ambayo kimsingi imemalizika.
Mbali na Israel kusitisha usambazaji wa Umeme, wiki iliyopita ilisimamisha pia upelekaji wa misaada Gaza kwa nia ya kulazimisha Hamas kuwaachilia mateka ambao inaendelea kuwashikilia.