Ujumbe wa Afrika waanza ziara Ukraine licha ya mashambulizi
16 Juni 2023Matangazo
Ujumbe huo wa viongozi wakiwemo marais kutoka Afrika Kusini, Senegal, Zambia, Visiwa vya Komoro na Misri, tayari umekutana na wawakilishi wa wizara ya ulinzi, kuelekea mazungumzo na Rais Volodymyr Zelenskiy yaliyopangiwa kufanyika baadae leo. Viongozi hao pia wanatarajiwa kukutana na Rais Vladimir Putin huko St.Petersburg hapo kesho, huku Kyiv na Moscow wote wakiiona nafasi hiyo kama fursa ya kusuluhisha vita hivyo ambavyo vimeziathiri nchi za Afrika hasa katika usambazaji wa nafaka na bidhaa zengine za chakula. Karibu miripuko miwili imeukumba mji wa Kyiv leo ila meya wa jimbo hilo Vitali Klitschko amesema imesababishwa na mifumo ya ulinzi.