Ujerumani: Rasimu mpya ya mpango wa fedha yawekwa wazi
15 Machi 2025Ujerumani imeweka wazi nakala ya rasimu ya sheria mpya inayohusu mpango maalumu wa fedha kwa ajili ya miundombinu na ulinzi wenye thamani ya dola bilioni 500 leo Jumamosi. Hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano kati ya muungano wa vyama ndugu vya Christian Democratic Union, CDU na Christian Social Union, CSU, unaoongozwa na Friedrich Merz anayetarajiwa kuwa Kansela, pamoja na chama cha Social Democtratic SPD na chama cha Kijani.
Soma zaidi.Starmer: Putin hana budi kuketi kwenye meza ya mazungumzo
Rasimu hiyo inabainisha kuwa mpango wa kulegeza ukomo wa serikali kukopa hautatumika kwenye masuala ya ulinzi pekee, bali pia kwenye matumizi ya serikali katika huduma za ujasusi, usalama wa mtandao, ulinzi wa raia na misaada kwa nchi ambazo zimeshambuliwa kinyume na sheria ya kimataifa.
Kulingana na nakala hiyo jumla ya euro bilioni 100 kutoka katika mfuko maalumu zitaongezwa katika mfuko wa sasa wa tabianchi na marekebisho ya uchumi yanayozingatia hali ya hewa rafiki.