Ujerumani yawatia nguvuni vijana waliopanga mashambulizi
21 Mei 2025Matangazo
Vijana hao pia wanadaiwa kupanga kuihujumu serikali. Waendesha mashtaka wa shirikisho wamesema washukiwa hao wenye umri wa kati ya miaka 14 na 18 walikuwa wanachama au wafuasi wa kundi hilo lililoasisiwa Aprili mwaka 2024.
Katika taarifa waendesha mashtaka hao wamesema lengo lao lilikuwa kuuangusha mfumo wa demokrasia katika Jamhuri ya Shirikisho ya Ujerumani kupitia machafuko.
Vijana hao wanadaiwa kuwa walikuwa wamepanga kufanya visa vya uteketezaji wa makaazi na taasisi za waomba hifadhi.