Ujerumani yawarudisha kwao raia 43 wa Iraq
23 Julai 2025Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imethibitisha kwamba raia 43 wa Iraqwalisafirishwa kwa ndege kuelekea mjini Baghdad siku ya Jumanne baada ya taarifa kusambaa kuhusu safari hiyo ambayo ni ya kwanza tangu safari ya ndege ya aina hiyo kufanyika mnamo Februari.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Alexander Donbrindt ambaye amekuwa akishinikiza msimamo mkali zaidi kuhusu uhamiaji amesema safari hiyo ya ndege ilikuwa sehemu ya sera mpya huku akiendelea kuitisha raia wengi zaidi warejeshwe nchini kwao, na kutaka makubaliano na nchi nyingine na hatua kali zaidi zichukuliwe kuwadhibiti wafanyabiashara haramu ya usafirishaji binadamu.
Kwa mujibu wa mamlaka katika jimbo la Thuringia wanaume wote 43 wa Iraq waliondokea uwanja wa ndege wa mji wa mashariki wa Leipzig na walikuwa wametakiwa waondoke Ujerumani.