Ujerumani yatoa wito uthabiti wa Syria usiyumbishwe
17 Julai 2025Matangazo
Ujerumani imetoa wito pawepo na hali ya kujizuia nchini Syria ili kuepusha kuhatarisha utulivu na nchi hiyo isigeuzwe kuwa uwanja wa mivutano ya kikanda.
Wito huo umetolewa hivi leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Johann Wadephul baada ya machafuko kuongezeka hapo jana wakati Israel ilipofanya mashambulizi iliyosema yalilenga kuwalinda watu wa jamii ya Druze nchini Syria.
Katika taarifa yake Wadephul amesema kwa kuzingatia mashambulizi ya kutokea angani ya Israel, yakiwemo dhidi ya mji mkuu wa Syria, Damasucs, wadau wote wa ndani na nje wanatakiwa wajizuie kuchukua hatua zinazoweza kuhatarisha uthabiti wa Syria na mchakato wa mpito.