MigogoroRwanda
Ujerumani yasitisha msaada mpya kwa Rwanda
5 Machi 2025Matangazo
Watalaamu wa Umoja wa Mataifa wanasema waasi hao wanasaidiwa na wanajeshi wa Rwanda. Taarifa kutoka wizara ya maendeleo ya Ujerumani itazuia ushirikiano zaidi wa pande mbili na Rwanda.
Mbali na kusitisha msaada mpya wa kifedha, wizara hiyo imesema itatathmini ushirikiano uliopo kwa sasa wa maendeleo na serikali ya Rwanda. Msaada wa wizara ya maendeleo ya Ujerumani kwa Rwanda ni wastani wa euro milioni 50 kwa mwaka.
Wizara ya mambo ya nje ya Rwanda imejibu kwamba Ujerumani "kuingiza siasa katika ushirikiano" ni "kosa na jambo lisilo na tija". Hatua ya Ujerumani imejiri baada ya Uingereza hivi karibuni kusitisha msaada wake wa moja kwa moja kwa Rwanda na Canada ikaiwekea vikwazo nchi hiyo kuhusiana na mzozo huo.