Ujerumani yashindwa kufuzu fainali ya Ulaya
24 Julai 2025Matangazo
Hii ni katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia Alhamis.
Mchezaji bora duniani kwa wanawake Aitana Bonmati ndiye aliyefunga goli hilo la pekee la Uhispania kunako dakika ya mwisho ya zile dakika thelathini za ziada, baada ya timu hizo mbili kumaliza dakika tisini zikiwa zimetoshana nguvu kwa sare ya kutofungana.
Hii ndiyo mara ya kwanza kwa Uhispania kuifunga Ujerumani baada ya timu hizo mbili kukutana mara mbili. Uhispania sasa itachuana na England katika fainali itakayochezwa Jumapili.
England ndiyo mabingwa watetezi huku Uhispania wakiwa ni mabingwa wa dunia. England walitinga fainali baada ya kuibwaga Italia 2-1 hapo juzi Jumanne.