UhalifuUjerumani
Ujerumani yarekodi visa 18,000 vya ukatili wa kingono
21 Agosti 2025Matangazo
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Ofisi ya Polisi ya Shirikisho ya Kupambana na Uhalifu nchini Ujerumani, BKA.
Idadi kubwa ya wahanga wa unyanyasaji wa kingono, picha za ngono kwa watoto na unyanyasaji wa kijinsia ni wasichana 13,365, huku visa 4,720 vikiwahusisha wavulana.
BKA imesema katika asilimia 57 ya kesi zote za unyanyasaji wa kingono, mtuhumiwa na mwathiriwa walikuwa wakijuana kabla ya tukio hilo kufanyika.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Alexander Dobrindt amesema sehemu kubwa ya makosa hayo yalifanyika mtandaoni.
Mwaka jana, idara ya polisi ilikuwa inachunguza kesi 16,354 za unyanyasaji wa kingono kwa watoto, bila ya kuwepo tofauti kubwa na kesi 16,375 zilizorekodiwa mwaka uliotangulia wa 2023.