Sheria na HakiUjerumani
Ujerumani yarefusha kipindi cha ukaguzi wa mipakani
12 Februari 2025Matangazo
Scholz amesema hayo kabla ya uchaguzi wa Fenruari 23, ambao umegubikwa na suala la wahamiaji na kuongeza kuwa ameagiza ukaguzi kufanyika kwenye mipaka yote ya Ujerumani na tayari ameiarifu Halmashauri Kuu ya Ulaya.
Scholz amesema kwamba tangazo hili lililotolewa hii leo linaonyesha nia yake ya kuendelea kusimama kwa uthabiti katika vita dhidi ya uhamiaji usio wa kawaida.
Soma pia:Masuala ya uhamiaji yatawala kampeni za uchanguzi Ujerumani
Scholz kutoka chama cha SPD amekabiliwa na shinikizo kubwa kuhusiana na suala hilo baada ya msururu wa mashambulizi makubwa yanayohusishwa na waomba hifadhi.
Amesema, watu 47,000 wamerudishwa makwao kufuatia ukaguzi huo wa mipakani hadi sasa.