Ujerumani yapitisha mpango wa ukomo wa ukopaji
19 Machi 2025Kansela anayeondoka wa Ujerumani Olaf Scholz ameusifu mpango wa ulinzi wa mabilioni ya dola uliopitishwa na bunge la Ujerumani jana, akisema ni mchango mkubwa kwa juhudi za ulinzi Uaya. Bunge la Ujerumani, Bundestag, liliidhinisha mpango wa kihistoria wa kulegeza kikomo cha ukopajicha Ujerumani kwa ajili ya kupiga jeki ulinzi na kutenga zaidi ya dola bilioni 500 kwa miundo mbinu na hatua za ulinzi wa mazingira. Mpango huo huo umepita kwa kura 512 dhidi ya 206 na ilikuwa inachukuliwa kama mtihani mkuu kwa Kansela mtarajiwa wa Ujerumani Friedrich Merz. Merz amesema fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya usalama wa Ujerumani, Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO. Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte pia amewapongeza Scholz na Merz kwa makubaliano hayo ya kihistoria.