Ujerumani yapinga kuwahamisha Wapalestina kutoka Gaza
27 Januari 2025Matangazo
Kauli hiyo imetolewa na wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani ambayo inaakisi pia msimamo wa Umoja wa Ulaya, nchi za kiarabu na hata Umoja wa Mataifa.
Haya yanajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuyataka mataifa ya Jordan na Misri kuwapokea wakimbizi wa Kipalestina kutokana na uharibifu wa miezi 15 ya vita huko Gaza.
Soma pia:Israel yawaruhusu wapalestika kurejea Kaskazini mwa Gaza
Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na kundi la Hamas wameapa kukaidi mapendekezo yoyote ya kuwaondoa Wapalestina huko Gaza.