Ujerumani yamtaka balozi wa Iran aeleze kuhusu ujasusi
1 Julai 2025Matangazo
Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imemuita balozi wa Iran atoe maelezo baada ya mwanamume mmoja kukamatwa kwa kushukiwa kufanya ujasusi kwa ajili ya Iran kwa nia ya kukusanya taarifa kuhusu maeneo ya kiyahudi na watu binafsi mjini Berlin.
Ofisi ya waendesha mashitaka ya Ujerumani mjini Karlsruhe imesema Jumanne kwamba mwanamume huyo raia wa Denmark alikamatwa nchini Denmark.
Katika taarifa yake wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema haitavumilia kitisho chochoe kwa maisha ya wayahudi nchini Ujerumani na madai dhidi ya mwanamume nchini Denmark kwamba alijifanya kama ni wakala wa ujasusi kwa ajili ya Iran lazima yachunguzwe kikamilifu.