Ujerumani yasaka kundi linalopanga kuiangusha Eritrea
26 Machi 2025Matangazo
Waendesha mashitaka wa Ujerumani wamesema washukiwa hao wanaaminika kushikilia nyadhifa kubwa katika kundi la Brigade N'Hamedu - tawi la Ujerumani, ambalo limekuwa likiendesha harakati zake tangu 2022.
Kundi hilo linaelezwa kuwa mtandao wa kimataifa na linajulikana kwa kutumia vurugu dhidi ya wafuasi wa serikali ya Eritrea. Linatuhumiwa kwa kupanga ghasia katika matamasha ya Kieritrea mjini Giessen, karibu na Frankfurt Agosti 2022 na Agosti 2023.
Pia kwenye warsha iliyoandaliwa na chama cha Kieritrea mjini Stuttgart mnamo Septemba 2023.
Karibu makazi 19 yamepekuliwa mapema leo nchini Ujerumani. Mpaka sasa hakuna aliyekamatwa.