Ujerumani yaingia siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi
22 Februari 2025Muungano wa upinzani wa vyama ndugu vya CDU/CSU unafanya mkutano wao wa mwisho leo mchana mjini Munich.
Watakaohutubia katika mkutano huo ni mgombea mkuu wa umoja huo na kiongozi wa CDU Friedrich Merz, ambaye ndiye anapigiwa upatu kuwa Kansela ajae wa Ujerumani.
Kampeni zakaribia kumalizika Ujerumani
Wengine watakaopanda jukwaani ni Kiongozi wa CSU Markus Söder, pamoja na mgombea mkuu waCSUAlexander Dobrindt. Hafla hiyo itafanyika faraghani chini ya ulinzi mkali.
Maandamano kufanyika katika miji kadhaa ya Ujerumani
Maandamano pia yamepangwa katika miji kadhaa ya Ujerumani hii leo kabla ya uchaguzi huo. Waandamanaji wanapinga baadhi ya sera za vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia katika maeneo kama Hamburg na Hanover, huku wakitoa wito wa kuvumiliana katika maeneo kama Kiel.