Ujerumani yaihimiza Israel kuondoa vikwazo vya misaada Gaza
10 Machi 2025Akirejelea uamuzi wa kusitisha msaada, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani Kathrin Deschauer aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba Gaza inakabiliwa tena na kitisho cha uhaba wa chakula na kwamba hatua kama hizo hazikubaliki na haziendani na wajibu wa Israeli chini ya sheria za kimataifa.
Amesema Ujerumani inatoa wito kwa serikali ya Israel kuondoa vikwazo vya aina zote kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza.
Soma pia: Israel yasitisha usambazaji wa umeme katika Ukanda wa Gaza
Awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas ilimalizika mwanzoni mwa mwezi Machi bila makubaliano yoyote juu ya hatua zinazofuata ambazo zingelenga kupata mwisho wa kudumu wa vita vilivyozuka na baada ya shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel.