Ujerumani yahamisha "wahalifu wa kigeni"
18 Julai 2025Matangazo
Hatua hii ni operesheni ya pili ya aina hiyo tangu utawala wa Talibanuliporejea madarakani.
Waziri wa Mambo ya Ndani Alexander Dobrindt alithibitisha kuwa ndege iliyowabeba raia hao wa Kiafghani tayari imeondoka, na kwamba wote walikuwa wameamriwa kuhamishwa baada ya kupatikana na hatia.
Ujerumani ilikuwa imesitisha uhamishaji wa raia kwenda Afghanistan na kufunga ubalozi wake mjini Kabul baada ya Taliban kurejea madarakani mwaka 2021, lakini serikali ya sasa ya Kansela Friedrich Merz imechukua msimamo mkali zaidi kuhusu uhamiaji, na imeanza tena uhamishaji wa wale wanaoitwa "wahalifu wa kigeni", ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kisiasa ya serikali ya mseto anayoiongoza.