MigogoroSudan Kusini
Ujerumani yafuunga kwa muda ubalozi wake nchini Sudan Kusini
23 Machi 2025Matangazo
Wiki hii, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alimfuta kazi gavana wa jimbo la Upper Nile, ambako mapigano yameongezeka kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa kikabila anaowatuhumu kushirikiana na mpinzani wake, Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar.
Msuguano huo umeongeza wasiwasi kwamba taifa hilo linaweza kurudi kwenye mzozo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua mamia ya maelfu ya watu.