Ujerumani yachuana na ureno kuania nafasi ya tatu ya kombe la dunia
8 Julai 2006
Na hatimae tuteremke kiwanjani mjini Stuttgart ambako leo usiku Ujerumani itashindana na Ureno kuania nafasi ya tatu ya kombe la dunia.Oliver Kahn atalinda lango la Ujerumani hii leo na atashika nafasi ya nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Michael Ballack aliyejeruhiwa.Hapo awali rais Thabo Mbeki wa Afrika kusini alisema wakati wa mazungumzo pamoja na kansela Angela Merkel mjini Berlin,nchi yake imeshapanga namna ya kuandaa michuano ya fainali la kombe la dunia mwaka 2010.Rais Thabo Mbeki amefurahishwa na utayarifu wa kamati ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Ujerumani,wa kuisaidia kamati ya maandalizi ya kombe hilo nchini mwaker.Shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA linapanga kutia njiani mpango wa kulisaidia bara zima la Afrika,wakati huu wa maandalizi ya kombe la dunia 2010.