Ujerumani, Uingereza kuongoza mkutano wa msaada kwa Ukraine
4 Juni 2025Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Rustem Umerov, anatarajiwa kuwahutubia washirika wa nchi yake kuhusu hali kwenye uwanja wa vita nchini humo pamoja na mahitaji muhimu zaidi.
Mkutano wa kilele kuhusu Ukraine huko Ramstein waahirishwa
Mazungumzo hayo ambayo awali yaliongozwa na Marekani, sasa yataongozwa na waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, na mwenzake wa Uingereza, John Healey.
Wanasiasa hao wawili wanajaza pengo la aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, ambaye alianzisha kundi hilo ambalo pia lilipewa jina na kuitwa Kundi la Ramstein, linalojumuisha takribani nchi 50, kabla ya mabadiliko ya serikali nchini Marekani.
Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte, pia anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari kabla ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa muungano huo mjini Brussels kesho Alhamisi.