Ujerumani, Ufaransa kujadili uchumi na ulinzi
29 Agosti 2025Matangazo
Mkutano huo utawashirikisha mawaziri 10 kutoka pande zote mbili. Hapo baadaye, baraza la pamoja la ulinzi na usalama litafanya mazungumzo kuhusu uzalishaji wa silaha na miradi ya pamoja ya ulinzi. Viongozi wa nchi za Ufaransa na Ujerumani wanafanya juhudi za kuimarisha ushirikiano baada ya uhusiano wa mashaka kati ya mtangulizi wa Merz, Olaf Scholz, na Rais Macron. Macron amesisitiza kuwa ushirikiano wenye mafanikio kati ya Ujerumani na nchi yake ni muhimu katika kuiimarisha Ulaya.