Ujerumani na Uingereza zasaini mkataba wa ushirikiano
17 Julai 2025Matangazo
Miaka mitano tangu Uingereza ilipojitoa kutoka kwenye Umoja wa Ulaya, nchi hiyo na Ujerumani zimeuweka uhusiano wao katika mkondo mpya kwa kusaini mkataba wa ushirikiano.
Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz na Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer wamesaini mkataba wa kurasa 27 unaoainisha mpango mkakati wenye vipengele 17, wakati wa hafla iliyofanyika katika jumba la makumbusho la Victoria na Albert jijini LondoN:
Merz ambaye anafanya zaira yake ya kwanza Uingereza amesema leo ni siku ya kihistoria kwa mahusiano kati ya Ujerumani na Uingereza.
Mkataba huo unanuia kuimarisha ushirikiano katika ulinzi, sera ya uchumi, uhamiaji na mapambano dhidi ya uhalifu kati ya mipaka.