Ujerumani/Uingereza kutia saini mkataba wa ulinzi wa pamoja
2 Julai 2025Matangazo
Mkataba huo unatarajiwa kutiwa saini Julai 17.
Ripoti hiyo imekuja takriban mwaka mmoja baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Kansela wakati huo wa Ujerumani Olaf Scholz, kutoa tamko la pamoja kuahidiana ushirikiano wa karibu zaidi katika masuala tofauti kuanzia bishara hadi usalama.
Jarida la Politico limesema ahadi hizo sasa zinafanyiwa kazi na suala linalopewa kipaumbele ni usalama.
Licha ya mataifa hayo mawili kuwa wanachama wa Jumuiya ya kujihami NATO, mkataba huo unaangazia mwelekeo mpya miongoni mwa nchi za Ulaya ikiwemo Ujerumani, ambayo sasa ipo chini ya utawala wa kansela Friedrich Merz, kufanya kazi pamoja na kujaribu kuondoa utegemezi kikamilifu wa Marekani chini ya rais Donald Trump.