Ujerumani kumpeleka Myemeni Marekani:
14 Novemba 2003Matangazo
BERLIN: Mahkama kuu ya Ujerumani imetoa ruhusa kumpeleka Myemeni Marekani kwa mashtaka ya ugaidi, baada ya Marekani kukubali kutomfungulia kesi kwenye mahkama ya kijeshi. Msemaji wa wizara ya sheria ya Ujerumani alisema uwamuzi wa mwisho utapitishwa karibuni baada ya kushauriana na wizara ya kigeni. Sheikh wa kiislamu wa Ki-yemeni Mohammed Ali Hassan Al Nouyad alikamatwa Ujeumani Januari, kufuatia kutolewa waranti na Marekani. Anatuhumiwa kuvisaidia kwa fedha na silaha, vyama vya kigaidi vikiwamo El Qaida na Hamas.