Ujerumani isiyo na mabeki kukabiliana na Uhispania
21 Julai 2025Haya ni kulingana na shirikisho la kandanda la Ujerumani, DFB.
Hilo sasa linaiweka Ujerumani ambaye ni bingwa mara nane katika nafasi ngumu hasa katika safu ya ulinzi kuelekea mechi hiyo dhidi ya timu hiyo inayopigiwa upatu kuunyakuwa ubingwa.
Beki huyo wa shoto anayeichezea klabu ya Wolfsburg, alipata jeraha la mguu wake wa shoto wakati wa mechi ya robo fainali dhidi ya Ufaransa, alipokuwa akipambania mpira na mshambuliaji Marie-Antoinette Katoto.
Shirikisho la kandanda la Ujerumani limesema haijabainika iwapo Linder atapona kwa wakati kuweza kushiriki fainali iwapo Ujerumani itawalaza Uhispania na kutinga hatua hiyo ya mwisho.
Kiungo Nüsken pia atakosekana kutokana na jeraha
Kabla ya jeraha hilo Ujerumani tayari ilikuwa inamkosa beki wa kulia Giulia Gwinn, nahodha wa timu hiy aliyepata jeraha la goti katika mechi ya ufunguzi.
Beki Kathrin Hendrich hatopatikana kwa mechi dhidi ya Uhispania kwa kuwa alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumvuta nywele mchezaji wa Ufaransa Griedge Mbock Bathy katika mechi ya robo fainali.
Kiungo wa kati Sjoeke Nüsken pia ana marufuku kwa kuwa alionyeshwa kadi yake ya pili ya njano katika mashindano hayo kwenye mechi dhidi ya Ufaransa.
Beki wa Bayer Leverkusen Carlotta Wamser, aliyeonyeshwa kadi nyekundi katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Sweden, huenda akarudi baada ya marufuku yake kuisha baada ya mechi dhidi ya Ufaransa.
Chanzo: AP