Daktari anaedaiwa kuwaua wagonjwa wazee achunguzwa Ujerumani
8 Julai 2025Polisi na waendesha mashitaka katika mji wa Itzehoe Kaskazini mwa Ujerumani wamethibitisha kuanzisha rasmi uchunguzi wa vifo vya wagonjwa hao wazee, kwa kuvichunguza upya vifo vilivyotokea awali vya wazee vilivyofungamanishwa na daktari huyo anaetokea mji wa Pinneberg Kaskazini mwa Ujerumani nje ya mji uliokaribu wa Hamburg.
"Uchunguzi na ufukuaji wa maiti tayari umefanywa na majibu yanatarajiwa kutolewa ndani ya wiki kadhaa zijazo. Polisi imeongeza kuwa haitoweka wazi idadi ya waliouwawa lakini imethibitisha kuwa wagonjwa wengi walioangamia walikuwa wazee.
Mzee akamatwa kwa tuhuma za kuanzisha moto hospitali Hamburg
Kisa hiki kimekumbusha sakata jengine lililotokea katika siku za hivi karibuni nchini Ujerumani lililowahusisha pia madaktari walioshitakiwa kwa makosa ya kuwaua wagonjwa kwa maksudi.
Mwezi Aprili, waendesha mashitaka mjini Berlin walimshtaki daktari mmoja kwa mauaji ya wagonjwa 15 wenye umri wa kati ya miaka 25 na 94.
Na mwezi Machi, muuguzi mwengine alifikishwa mahakamani mjini Aachen akituhumiwa kuwadunga wagonjwa 26 dozi kubwa ya dawa za kupunguza maumivu hatua iliyosababisha vifo vya wagonjwa 9 kati ya hao 26.