"Ujerumani inakumbuka utamaduni wake"
17 Januari 2006“Bibi Angela Merkel anaonekana kama anaangalia matatizo kwa kutafuta suluhisho badala ya kubaki na mzozo tu. Baada ya ziara yake nchini Marekani na wakati wa kurudi kutoka Russia, siasa ya mambo ya nje ya Ujerumani inakumbuka tena utamaduni wake, yaani ni kuzuia kuingiza katika hali ambapo ni lazima kuchagua baina ya Marekani na Ufaransa kama katika mzozo wa Irak. Wakati huo Ujerumani iliunga mkono na Ufaransa na Russia dhidi ya msimamo wa Marekani.”
Na mhariri wa gazeti la “Westdeutsche Zeitung” anasifu sera ya Kansela Angela Merkel:
“Bi Merkel anafanya vizuri kwa kutaja shida zilizopo bila ya kuukera upande mwingine. Vile vile anafanya vizuri kwa kutochukua msimamo mkali, lakini badala yake kuchukua nafasi ya mpatanishi kama inavyofaa mamlaka yasiyo muhimu kabisa wala chini kabisa. Ukiangalia mizozo mipya kama kwa mfano ule wa Iran, nafasi ya mtapanishi inaweza kuleta faida kubwa. Sera mpya ya Angela Merkel ni njia ya zamani. Na waziri wa mambo ya nje, Frank-Walter Steinmeier, hawezi kupinga mwenendo huo. Juu ya hayo hana nguvu ya kutosha kufanya hivyo.”
Na gazeti la “Süddeutsche Zeitung” linazingatia hasa upande wa uchumi katika mahusiano baina ya Ujerumani na Russia:
“Bado Bibi Merkel hajaonyesha ikiwa ataweza kukataa kufuata amri ya mameneja wa Ujerumani. Baadhi ya yake watajaribu kumfahamisha Merkel kwamba ni lazima aiunge mkono serikali ya Russia ili uchumi wa Ujerumani uweze kufanya biashara nzuri. Ukweli ni kwamba inabidi kuna usawa wa nguvu kama Bibi Merkel anavyoonyesha: Ujerumani inaweza kufuata maslahi yake nchini Russia katika hali ya ushirikiano bila ya kuondosha malengo yake ya kidemokrasi.”
Mada nyingine inayozungumziwa na wahariri wa magazeti ni mzozo wa Iran. Kama ulivyosikia katika matangazo yetu hivi punde tu, bado haijaamuliwa ni hatua gani zitakazochukuliwa ili Iran imalize mradi wake wa kinyuklia. Kuhusu suala hilo, gazeti la “Badische Zeitung” lina haya ya kusema:
“Ikiwa kwa kweli Iran inatishiwa na vikwazo vya kiuchumi, labda ingefikiria upya sera yake. Kwa bahati mbaya lakini nchi kama Russia na China hazitaki kutoa amri hiyo. Je, ni lazima sasa nchi za Ulaya zinalazimishwa kuangalia tu Iran kuendelea na mradi wake wa kinyuklia bila ya kuweza kufanya chochote dhidi yake? Hapana! Iran ina mahusiano mengi ya kiuchumi na nchi za Ulaya, kwa hivyo Umoja wa Ulaya unaweza kuweka vikwazo vyake vya kiuchumi bila ya kusubiri baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Bila shaka hakuna uhakika ikiwa hatua hiyo inaisababisha Iran kubadilisha msimamo wake, lakini ingefaa kujaribu.”
Katika maoni yake, mhariri wa gazeti la “Tageszeitung” anaandika:
“Uwezekano wa kuepukwa kwa vita vingine katika eneo la Mashariki ya Kati haupo mbele tena. Hali ya hivi sasa inafanana na hali kabla ya vita dhidi ya Irak. Lakini kuna tofauti muhimu: Safari hii siyo Marekani na Uingereza peke yao zinazopinga Iran. Baada ya kushindwa katika jitihada zao za kidiplomasia, Umoja wa Ulaya unaziunga mkono. Sasa inabidi kuondolea Russia na China mashaka yao ya kuweka vikwazo va kiuchumi dhidi ya Iran. Tofauti nyingine ni kwamba Iran siyo Irak. Licha ya Wairan wengi kupinga serikali yake, baado mamillioni ya raia wa Iran wanaiunga mkono. Kushambulia Iran kutoka nje kutasababisha ushirikiano mzito pamoja na upinzani mkali dhidi ya nchi za Magharibi.”