Ujerumani yaachukua wakimbizi 942 chini ya mpango wa Ulaya
19 Agosti 2025Wakimbizi hao wanatoka Sudan, Syria, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Eritrea na nchi nyingine kadhaa. Hata hivyo, tangu serikali mpya ilipoingia madarakani Mei 7, mwaka huu, hakuna watu zaidi walioingia Ujerumani.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani imesema makubaliano ya serikali ya muungano kati ya vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU na Social Democratic, SPD, yanataka programu za kuwasaidia watu wanaotoka kwenye maeneo ya mizozo isitishwe, na kutoanzishwa mipango mingine mipya.
Chini ya mpango huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, linawatambua hasa watu walio hatarini kupata makaazi mapya.
Mamlaka ya Ujerumani kisha inafanya mahojiano na kukagua usalama katika maeneo. Wakimbizi hawahitaji kuwasilisha barua ya kuomba hifadhi pindi wanapowasili Ujerumani.